8/17/2020

RPC Morogoro afunguka ajali ya Kontena kukandamiza Costa


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa jumla ya watu 10 wamejeruhiwa huku 4 kati yao wakijeruhiwa vibaya, baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kukandamizwa na Kontena ambalo lilikuwa limebeba Tumbaku katika eneo la Nanenane mkoani humo hii leo.Kamanda Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo imetokea hii leo Agosti 17, 2020 majira ya saa 3:00 asubuhi, ambapo gari aina ya Costa ilikuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro na ndipo ilipolivagaa Lori hilo ambalo lilikuwa limepata hitilafu iliyopelekea Tela lake kukatika na hivyo kuziba njia yote."Tela hilo lilikatika hivyo kusababisha Tela lililokuwa limebeba tumbaku kukata barabara yote na ndipo gari aina ya Costa iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam iliweza kuingia ubavuni kabisa mwa hilo Tela, tumeokoa jumla ya watu 6 wamepelekwa Hospitali na hali zao ni nzuri, lakini pia tumetoa watu 4 ambao walikuwa mbele kabisa na walikuwa wamekandamizwa na hali zao ni mbaya" amesema Kamanda Mutafungwa.Aidha Kamanda Mutafungwa amesema kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger