8/24/2020

Sauti za Vuja Akisikika Dada wa Trump Akimsema Kaka yake Kuwa ni "Muongo" "Mkatili" na Asiepaswa KuaminiwaWashington Dada wa rais wa Marekani Donald Trump amemuelezea rais huyo kama mkatili na muongo na asiyepaswa kuaminiwa, hii ikiwa ni kwa mujibu wa sauti yake iliyorekodiwa kisiri na kuchapishwa jana Jumamosi.

Hili ni tukio la hivi karibuni kumlenga rais Trump lakini sio kutoka kwa mahasimu wake wa kibiashara au kisiasa lakini kutoka kwa jamaa yake wa karibu ambae ni dadake Maryanne Trump Barry.

Maryanne amemkosoa kakake Trump juu ya sera zake za kigeni zilizowafanya watoto kutenganishwa na wazazi wao mipakani na kupelekwa vizuizini.

Amesema kile anachotaka ni kujisifia, hana misingi ya uongozi na jumbe zake katika ukurasa wa twitter ni za uwongo, alisema Maryanne katika sauti ilionaswa na Washington Post iliorekodiwa na mpwa wa Trump Mary Trump.Hata hivyo ikulu wa White House imetoa taarifa kutoka kwa Trump inayosema " kila siku ni kitu kipya, hajali na ataendelea kufanya kazi kwaajili ya watu wa Marekani na kwamba Marekani hivi karibuni itakuwa imara zaidi kuliko ilivyokuwa zamani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger