8/10/2020

Serikali Yaruhusu Kusajili Wachezaji 10 wa Kigeni


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu vilabu vya soka nchini kuendelea kusajili wachezaji 10 wa kigeni, hatua iliyochukuliwa baada ya kuzingatia maoni ya wadau.

Akitangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Agosti 10, 2020, Waziri mwenye dhamana ya michezo, Dkt. Harison Mwakyembe ametsema idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuanza kucheza itabaki chini ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Pia amesema bado wizara kwakushirikiana na BMT na wadau wa soka watakaa kitako kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia kucheza nchini.

“”Ni vyema pia aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka Nje wawe na weledi, wawe na uwezo mkubwa. Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndiyo tusajili huko hata wa daraja la kwanza, ingawa bado hii si sheria ni maoni tu,” amesema Mwakyembe.

Amesema kati watu 977 waliyotoa maoni, watu 809 wametaka idadi ya wachezaji 10 wakigeni. Kando na hayo Wizara imeagiza watu wanaoajiriwa nchini wawe na ulazima wa kujifunza / kufunzwa lugha ya Kiswahili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger