8/23/2020

Sevilla Yaichomolea Yanga SC


YANGA ipo katika taratibu za mwisho kukamilisha mipango ya kuileta moja ya klabu kubwa kutoka nchini Burundi kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafi ki kabla ya Ligi Kuu Bara baada ya kushindikana kuwaleta Sevilla FC ya nchini Hispania.

Yanga imepanga kuileta timu hiyo katika kilele cha Wiki ya Mwananchi kwa ajili ya kucheza mchezo huo Agosti 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa maambukizi ya Covid 19, ndiyo yamesababisha washindwe kuwaleta Sevilla.

Bumbuli alisema baada ya kushindikana kuwapata Sevilla wakahamia kwa nchi za Afrika Magharibi kwa ajili ya kuileta moja ya timu kubwa itakayonogesha tamasha lao hilo.

Aliongeza kuwa napo Afrika Magharibi ilishindikana kuipata timu kutokana na Covid 19 ambayo imeonekana kushika kasi katika ukanda wa nchi zao kabla ya kurudi Burundi ambako maambukizi yamepungua.

“Moja ya klabu kubwa ya nchini Burundi ndiyo itakayokuja nchini kwa ajili ya kucheza nayo mchezo wa kirafi ki katika siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi.


“Tulipanga kuileta Sevilla lakini imeshindikana kutokana na Covid 19, hivyo upo uwezekano wa kuileta timu hiyo kubwa nchini Hispania, mwakani tukiwa katika maandalizi ya kuanza msimu mpya,” alisema Bumbuli
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger