Shilole aonyesa nyumba yake "Pambana uwe na cha kwako, hata kama ni kidogo"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msanii wa muziki nchini, Shilole ameonyesa nyumba yake iliyoko Majohe, Dar es Salaam ambayo imekamilika kwa sasa.

Mwimbaji huyo amefanya hivyo kama kutoa motisha kwa wasichana kama yeye kupambana ili kuweza kumiliki vitu vyao wenyewe.

“Pambana uwe na cha kwako, hata kama ni kidogo, ongeza nidhamu yako ya fedha, kubali wakuite mbahili, wekeza kidogo kidogo. Mungu akusaidie ununue kakiwanja kako mahali, jenga taratibu, nyumba itakusitiri wakati wote,” ameandika Shilole kwenye ukurasa wake wa #Instagram.

Ikumbukwe mwaka jana wakati nyumba hiyo inaelekea kukamilika #Shilole alieleza kuwa ametumia zaidi ya Tsh. Milioni 90 ikiwa bado haijaweka vioo, kupakwa rangi n,k.


Aidha, Ujenzi huo ambao ulianza zaidi miaka minne iliyopita, Shilole alisema fedha zake alizipata kwenye muziki na hakuwahi kukopa ili kufanikisha hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad