8/18/2020

Shilole "Baba Levo Akishaka SIMU yangu Anaingia Asipotakiwa Kuchunguza Nimempata Nani"


Msanii mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa Shilole amefunguka kuwa msanii Baba Levo amekuwa akishika simu yake mara kwa mara kumchunguza kama amepata mwanaume mwingine.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital amesema, Baba Levo simu yake huwa haina bundle,  hivyo hutumia ya kwake ambapo akishaichukua anakuaga ujumbe wa kawaida na ujumbe wa Instagram "DM" ili kujua kama amepata mwanaume mwingine anayewasiliana naye.

"Mimi na Baba Levo tumezoeana sana, mara nyingi huwa anapoteza simu na simu yake inakuwa haina  vifurushi hivyo anataka kuingia Instagram aone, kwa hiyo nikimpa simu yangu huwa anaanza kukagua ili kujua nimempata nani au wakina nani wanatuma meseji za kutaka usajili mpya, bahati nzuri sina mambo mabaya kwenye simu yangu" ameeleza Shilole

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger