8/31/2020

Shujaa wa 'Hotel Rwanda' akamatwa kwa tuhuma za ugaidiMwanamume ambaye jukumu lake la kuwaokoa Wanyarwanda dhidi ya mauaji ya kimbari liliangaziwa katika filamu ya Hotel Rwanda,amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi.


Paul Rusesabagina amekamatwa ughaibuni ambako alikuwa anaishi mafichoni.


Shirika la upelelezi la Rwanda linasema alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa kwa kuunda na kuongoza "vuguvugu la kigaidi" linaloendesha shughuli zake katika eneo hilo.


Bw. Rusesabagina, 66, alitunukiwa medali ya Rais wa Marekani ya Uhuru 2005, miongoni mwa tuzo zingine za haki za binadamu.


Hajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma za sasa dhidi yake lakini amekuwa mkosoaji wa serikali ya Rwanda.


2011, alituhumiwa kuwafadhili wajumu wa serikali ya Rwanda, lakini hakufunguliwa mashitaka yoyote.


Wakati huo, Bw. Rusesabagina alipinga tuhuma dhidi yake na kudai ilikuwa njama ya kumharibia sifa.


Mwaka 2004 filamu ya Hotel Rwanda iliangazia jinsi Bw. Rusesabagina, Mhutu wa aliyemuoa mwenye Tutsi, alivyotumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashinikiza maafisa wa kijeshi kumpatia njia salama ya kuwatorosha karibu watu 1,200 kutafuta makazi katika Hoteli ya Mille Collines mjini Kigali.


Kundi la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka liliwahi kusema kuwa alitilia chumvi jukumu lake la kuwasaidia wakimbizi kujificha hotelini hapo siku 100-ya mauaji ya kikatili mwaka 1994.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger