8/05/2020

Simba Queens Kutangaza Ubingwa LeoSIMBA Queens huenda ikatangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu endapo itaibuka na ushindi mbele ya Baobab Queens leo.

Simba itavaana na Baobab Queens kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ambao utapigwa Dimba la Uhuru leo.

Simba Queens wapo kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 12, akiwa na jumla ya pointi 50, hivyo wanahitaji pointi tatu ili wakae kileleni wakiwa na pointi 53 ambazo haziwezi kufikiwa na bingwa mtetezi JKT Queens ambaye kabla ya mchezo wake wa jana dhidi ya TSC alikuwa na alama 43 sawa na Alliance Girls aliyecheza jana na Yanga Princess.

Simba Queens wamebakiza mchezo mmoja wa nyumbani, ambao ndiyo huu wanaocheza leo, kisha baada ya hapo watapaa hadi Kanda ya Ziwa pale jijini Mwanza kucheza michezo miwili dhidi ya Alliance Girls na TSC Queens na hiyo ndiyo itakuwa michezo yao ya mwisho kwa msimu huu.

Kocha wa Simba Queens Mussa Hassan (Mgosi) alisema kuwa:“Tunaiyona nafasi ya kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi ya msimu huu kama tukifanikiwa kushinda mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya Baobab, kwa sababu ukiangalia wenzetu wanaotufuta tumewaacha mbali hivyo itakuwa ngumu kutufikia, tuendelee kumuomba Mungu.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger