8/14/2020

Simba Yaanza Kuweka Hadharani Nyota Wake WapyaMabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam imemtambulisha mshambuliaji wake mpya, Charles Ilanfya aliyesajilia kutoka KMC .


Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Simba, Charles Ilanfya (Kulia pichani) akipokea Mkataba kutoka kwa Kocha msaidizi wa mabingwa hao wa Nchi , Seleman Matola (Kulia Pichani).

Nyota huyo ambaye aliwahi kuichezea Mwadui ya Shinyanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo ya soka hapa nchoni Tanzania.

Kabla ya kujiunga na Simba, Ilanfya ameitumikia KMC kwa msimu mmoja, ingawa kabla ya kutua KMC aliwahi kuwaniwa na Klabu ya Yanga kufuatia mapendekezo ya aliyekua kocha wa kipindi hiko Mwinyi Zahera lakini mpango hup haukukamilika.

Katika taarifa ya Klabu ya Simba, kupitia mitandao yake ya kijamii, imearifu kuwa usajili huo ni kutokana na mapendekezo ya kocha wao mkuu Sven Vandenbroeck ambaye alisema kuwa Ilanfya atakua msaada mkubwa kwa timu yao na Taifa kwa ujumla.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger