Sirro aomba wanasiasa wakemewe kwa hili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta  wa Polisi Simon Sirro, amewaomba viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya kukaa kimya.

Ametoa ombi hilo leo Agosti 22, 2020 akiwa anaongea na viongozi wa dini visiwani Zanzibar, kuhusuiana na suala la amani, katika kipindi chote cha uchaguzi ambapo amesema viongozi wa dini ni moja ya wadau wa amani nchini.

"Niwaombe sana kwasababu mnasikia baadhi ya maneno yanayotamkwa na baadhi ya wanasiasa lakini mmekaa kimya hamsemi, mmekaa kimya hamkosoi, mmekaa kimya mekuwa woga niwaombe sana ni muda sasa kuona kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tulikemee", - alisema IGP Sirro.

Aidha IGP Sirro amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini hawako kwa ajili ya kusaidia watanzania badala yake wapo kwasababu ya tama waliyonayo ya kutaka madaraka .

Hata hivyo IGP Sirro amewaonya viongozi wote wa dini wanaojihusisha na uhalifu kuwa atawachukilia hatua bila kujali nafasi yao katika jamii kwani ukikiuka sheria lazima uadhibiwe kwa mujibu wa sharia.

"Padri ukishajiingiza kwenye uhalifu mimi ntakushughulikia kama uhalifu mwingine, Padri ukishakuwa mbakaji ntakugonga kama mbakaji mwingine, Shehe/Padri ukijiingiza kwenye ugaidi ntakushughulikia kama gaidi hiyo kwasababua heshima ina ukubwa zaidi kuliko mtu binafsi" alisema IGP Sirro.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad