8/28/2020

Tanzania Yatoa Ufafanuzi Suala la Ndege 3 za Kenya


Mamlaka ya Usimamizi wa Anga nchini (TCAA), imesema kuwa sababu iliyopelekea kuzifungia Ndege 3 za Kenya kuja nchini inatokana na Nchi ya Kenya kuendelea kuiwekea vikwazo vizito Tanzania na raia wake kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Agosti 27, 2020, na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, ambapo ameongeza kuwa watafanya hivyo mpaka pale Kenya itakapoamua kufanya mazungumzo ili kumaliza suala hilo.

"Tumezifungia Ndege za Kenya kwa sababu Tanzania bado inawekewa vikwazo vizito kule kwahiyo na sisi tumerithishwa guility bila sababu",  amesema Mkurugenzi wa TCAA.
"Ili kumaliza hili suala ni mazungumzo tu na wao watakapokuwa tayari sisi tutakuwa tayari kwa mazungumzo maana sisi hatuna tatizo la kuzungumza na kuweka mambo sawa  lakini lazima wao wawe na utashi wa kufanya hivyo", ameongeza.

Ndege zilizowekewa zuio ni Air Kenya Express, Fly 540 na Safarilink Aviation, hatua hii inakuja ikiwa ni siku chache tu tangu Kenya ilipotoa orodha ya nchi 130 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini humo na hawatokaa karantini huku Tanzania ikiwekwa kando.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger