TB Joshua: Nasubiri Sauti Kutoka kwa Mungu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MCHUNGAJI maarufu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua,  anasema anasubiri kusikia ‘sauti ya Mungu’ kabla hajafungua huduma za ibada katika jiji la biashara la Lagos.

Mamlaka mjini Lagos imeruhusu huduma ya ibada kuanza siku ya Jumapili, waumini wakiwa nusu yake baada ya kufungwa kwa huduma hizo kwa miezi kadhaa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Katika video aliyoiweka kwenye kurasa yake ya Twitter, TB Joshua alisema amesikia sauti kutoka kwa mamlaka lakini bado anasubiri kusikia kutoka kwa Mungu.

“Muwe na uhakika kuwa punde tu nitakaposikia sauti ya Mungu, nitawajulisha huduma za ibada zitaanza lini,” aliongeza.

Mapema mwaka huu nabii huyo alisababisha mkanganyiko baada ya kudai kuwa mlipuko wa virusi vya corona utaisha Machi.27,  2020, siku chache kabla ya marufuku ya kutoka nje haijaanzishwa katika jimbo la Lagos, Ogun na mji mkuu Abuja.

“Mwishoni mwa mwezi huu, tupende au tusipende, haijalishi kama dawa gani itatengenezwa kwa ajili ya kutibu, virusi hivi vitaondoka kama jinsi vilivyokuja,” alisema hayo katika mahubiri yake.

Tarehe 27 Machi ilipopita alijikuta anadhihakiwa kwa maono ya uongo. Lakini alijitetea kwa kusema kuwa alimaanisha virusi vitaanza kuisha kule vilipoanzia, yaani  mjini Wuhan nchini China, na tayari vimeondoka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad