8/26/2020

TCRA kujenga Kiwanda cha Kuzalisha SimuSerikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema ifikapo Agosti mwakani itakuwa imeanzisha kiwanda cha kuzalisha simu janja ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu na kuwawezesha watanzania kuzitumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo elimu na biashara.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi James Kilaba amesema haya Jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari , mara baada ya kufunguliwa mafunzo ya majuma matano, kwa Mafundi simu wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini yanayolenga kuwajenga uwezo.


Aidha Mhandisi James kilaba ameeleza umuhimu wa Mafundi simu katika kuchangia pato la Taifa.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Albert Chalamila amefungua mafunzo haya na kudai kuwa uwekezaji uwekezaji unaofanywa na TCRA utakuwa na tija kwa Watanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger