Timu nzuri hazihitaji kusajili sana – Mo Dewji atupa dongo gizani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba Mo Dewji, ameonekana kama vile amerusha jiwe gizani kwa kusema kua timu nzuri hazihitaji kusajili sana.




Mo ameyasema hayo kipindi hiki ambacho timu mbalimbali zipo katika usajili katika kujiimarisha na michuano itakayo wakabili.




Katika ujumbe wake kwa mashabiki wa soka nchini, Mo ameandika ”Timu nzuri hazihitaji kusajili sana! #DirishaLaUsajili.”


Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuwa Simba SC imesajili mchezaji wowote yule tangu dirisha la usajili kufunguliwa tarehe 1 ya mwezi huu.


Maneno ya Mo ni kama amerusha dongo gizani kwakuwa upande wa pili kwa hasimu wao Yanga mpaka sasa wameshatangaza kusajili jumla ya wachezaji wanne mpaka taarifa za hapo jana siku ya Jumatatu ikiwa ni usajili uliyofanyika ndani ya siku tatu pekee tangu kufunguliwa kwa pazia la usajili ambalo litafungwa Agosti 31 saa 5:59 usiku.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad