8/28/2020

Trump amshambulia Joe BidenRais Donald Trump amemshambulia Joe Biden kuwa ameingia katika siasa kwa bahati mbaya na kwamba atahatarisha usalama wa Marekani. 


Ameyasema hayo wakati akikubali uteuzi wa chama chake katika hotuba aliyoitoa akiwa katika Ikulu ya nchi hiyo ya White House jana.


Wakati janga la virusi vya corona linawauwa Wamarekani 1,000 kila siku, Trump alikaidi miongozo ya utawala wake kupambana na janga hilo na kuzungumza kwa zaidi ya saa moja mbele ya kundi la watu waliokaa kwa kukaribiana, ambao kwa sehemu kubwa hawakuvaa barakoa.Akikabiliwa na hali ya mtafaruku wa ubaguzi, kuporomoka kwa uchumi na dharura ya kiafya ya taifa, Trump alitoa mtazamo wa ushindi na matumaini kwa hali ya baadae ya Marekani. 


Lakini alisema matumaini hayo yanaweza kupatikana iwapo atamshinda mgombea wa chama cha Democratic, ambaye kwa sasa anaongoza katika uchunguzi wa maoni katika majimbo muhimu na taifa kwa jumla.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger