8/02/2020

Tunda Afungukia Timbwili Aliloanzisha Whozu Baada ya Kumfumani LIVE na Young Dee

Tunda afungukia timbwili aliloanzisha Whozu baada ya kumkuta mazoezini na Young Dee

“Unajua mimi na Whozu siyo wapenzi kivile, tena kama ilivyokuwa zamani. Niliamua kwenda zangu kwa David (Young Dee) kwa sababu ni mshikaji wangu na alikuwa mtu wangu. Nilipokwenda kwake, alinipeleka mazoezini maana nimeongezeka sana unene,” Tunda ameiambia Globalpublishers

Tunda anaendelea kufunguka kuwa, wakiwa mazoezini huku Young Dee akimfanyisha mazoezi ya kumnyoosha viungo, ndipo alipoibuka Whozu, tena akiwa na nguo ya kulalia na kuibua timbwili la hatari.

“Yaani huwezi kuamini, wakati Young Dee ananifanyisha mazoezi, sijui hata Whozu alitokea wapi, akaanza kufanya fujo, tena amevalia nguo ya kulalia.
“Mimi niliona kama mapichapicha baada ya kumuona akichukua simu ya Young Dee na huwezi kuamini, kwani aliivunja kiasi kwamba haitamaniki kabisa,” anasema Tunda.

Mrembo huyo anasema kuwa, anamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwani Whozu hakuligusa gari ya Young Dee lililokuwepo eneo hilo la tukio.

“Ninamshukuru sana Mungu kwa sababu kwa hasira alizokuwa nazo Whozu, sijui nini kingetokea baada ya kuvunja simu, kwani nilijua kinachofuata ni kuvunja vioo vya gari na hapo mambo yangekuwa ni mengi mno,” anasema Tunda ambaye kwa sasa inasemekana amerejesha penzi lake rasmi kwa Young Dee.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger