Tundu Lissu Kuanza Safari yake ya Urais leo Dodoma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Leo Agosti 8, 2020 Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA Tundu Antipas Lissu, atafika katika ofisi za NEC Jijini Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa katika nafasi hiyo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, amesema zoezi  la kuchukua fomu litaambatana na shughuli za kutafuta wadhamini ambapo leo wataanzia katika ofisi za kanda ya kati zilipo jijini Dodoma.

Makene amesema kuwa baada ya shughuli zote hizo kumalizika,Kesho Agosti 9, 2020 watahamia katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kutafuta wadhamini, lakini pia itahusisha ujio wa Lissu katika eneo alilozaliwa tangu alipoondoka baada ya kushambuliwa na risasi.

“Shughuli zitaanza leo hakuna kitu kitalala na baada ya kuchukua fomu tutatafuta wadhamini ambapo leo ni hapa Dodoma baada ya hapo tutahamia Singida, tutatafuta wadhamini na pia ni ‘home coming’ ya Tundu Lissu na itakuwa ni siku mbili mana ni nyumbani baada ya jaribio la mauaji dhidi yake’’amesema Makene.

Zoezi hilo litahusisha viongozi na wanachama  wa CHADEMA ambapo Tundu Lissu ataambatana na Mgombea Mwenza Salum Mwalim pamoja na wananchi wengine watakaojitokeza
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad