Twitter Yazuia Akaunti ya Kampeni ya Rais Trump

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



TWITTER imezuia akaunti ya kampeni ya Rais wa Marekani,  Donald Trump, kwa kukiuka sheria zake zinazohusu usambazaji wa taarifa za upotoshaji, baada ya kuposti video ya rais huyo wa Marekani akisema watoto wana kinga dhidi ya Coronavirus.

Twitter imesema kuwa tweet kutoka akaunti ya @TeamTrump, ambayo ilionyesha video ya rais huyo katika mahojiano na kituo cha Fox News, “Iliukiuka sheria za Twitter juu ya taarifa za kupotosha kuhusu COVID-19″

Aidha, msemaji wa Twitter ameeleza kuwa mmiliki wa akaunti hiyo atalazimika kuondoa video hiyo kabla ya kurejeshewa uwezo wa ku-tweet tena.

Hatua hiyo ya Twitter imekuja masaa machache baada ya Facebook kuiondoa video hiyo hiyo kutoka kwenye akaunti binafsi ya Donald Trump.

Facebook ilichukua hatua hiyo kwa maelezo kuwa inahusisha madai ya uongo kwamba kundi fulani la watu lina kinga dhidi ya COVID-19, jambo ambalo ni ukiukaji wa sera za mtandao huo kuhusu taarifa zihusuzo ugonjwa huo

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad