8/17/2020

Uchunguzi wa mlipuko Lebanon utachukua muda mrefu – Rais Michel Aoun


Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema uchunguzi kuhusu mlipuko mkubwa uliotokea mapema mwezi huu mjini Beirut na kuwauwa watu 180 na kujeruhi maelfu wengine ni mgumu na huenda hautokamilika haraka.Katika mahojiano na kiuto kimoja cha televisheni cha nchini Ufaransa, Auon amesema uchunguzi huo umegawanywa kwenye hatua tatu na utahitaji muda zaidi kuweza kubaini kikamilifu kilichotokea kabla ya kufikia hitimisho.

Akijibu kuhusu shinikizo la kumtaka kujiuzulu kutokana na madai ya uzembe, Aoun amesema suala hilo haliwezekani kwa sababu litaacha ombwe la uongozi nchini humo.

Hadi sasa chanzo cha moto uliozuka kwenye ghala lililohifadhi maelfu ya tani za milipuko katika bandari ya Beirut bado hakijulikani. Duru kutoka Lebanon zinasema viongozi wa juu wa nchi hiyo akiwemo rais Aoun walifahamu uwepo wa hifadhi hiyo ya milipuko lakini hawakuchukua hatua.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger