8/07/2020

Umaarufu Kimuziki, Michezo Unavyowainua Wasanii Kisiasa


ZAMANI kazi ya michezo na muziki zilikuwa zinaonekana ni za kihuni na wazazi au walezi wa watoto walikuwa hawakubali vijana wao kuingia huko lakini sasa fani hizo ni mtaji mkubwa wa kuinua maisha kwa watu wa rika mbalimbali.

Kwa sasa vijana wetu wamepenya na kulishika soko la muziki Afrika Mashariki na kudhihirisha kuwa vipaji vinalipa hasa kwa baadhi ya vijana ambao ni wasanii wa Bongo Fleva lakini pia kuna watu wameinuka kisiasa kutokana na muziki au michezo.

Wafuatao ni wanamuziki na wanasiasa waliojipatia umaarufu na fedha nyingi kutokana na kazi ya muziki na wengine kujiingiza kwenye siasa na kupata mafanikio makubwa:

JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’

Joseph Mbulinyi au Sugu ni sasa ni mwanasiasa na ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva nchini. Wakati anauanza muziki huo hakueleweka na alionekana anaingiza uhuni tu katika jamii.

Lakini sasa amefanya muziki huu kwa takriban miongo miwili na kujipatia mafanikio makubwa. Kabla ya kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sugu alijiingizia fedha nyingi kupitia kuuza muziki na shoo mbalimbali.

Mwandishi wa makala haya aliwahi kuzungumza na Sugu akasema akiwa anafyatua albamu zake aliamua kuuza mwenyewe baada ya kugundua kuwa mawakala walikuwa wakimpunja kimapato. Alipofanya hivyo alijikuta akivuna mamilioni ya fedha.

Aliingia katika siasa na baada ya kukwaa ubunge mwaka 2010, Sugu aliendelea na muziki ambapo amekuwa akipiga shoo mojamoja kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wa masikini jimboni kwake Mbeya.

Muziki umemfanya Sugu amiliki mjengo wa kifahari jijini Mbeya alioupa jina la Khaki House. Pia kuna taarifa kuwa anamiliki mjengo mwingine jijini Dar. Mbali na mijengo hiyo, Sugu anamiliki hoteli ya kitalii ya nyota tatu iitwayo Desderiajijini Mbeya.

Kuhusu usafiri anaomiliki, baada ya kuwa mbunge anatembelea gari kali aina ya Toyota Land Cruiser V8 na magari mengine ya kawaida anayo.

JOSEPH HAULE ‘PROFESA JAY’

Kama ilivyo kwa Sugu, Jay ni miongoni mwa wasanii wakubwa walioupaisha muziki wa Bongo Fleva na kumfanya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Joseph Warioba kumsifia alipotoa ngoma kuwapa madongo wanasiasa kama ngoma ya Ndio Mzee.

Ngoma kama Chemsha Bongo, Nikusaidiaje na kadhalika licha ya kumuingiza fedha, zilikonga nyoyo za wananchi, Katika kipindi chote alichofanya muziki huo kabla ya kuwa Mbunge wa Mikumi kupitia Chadema mwaka 2015, Jay aliuza muziki na kufanya shoo nyingi kubwa ndani na nje ya nchi zilizomuingizia fedha nyingi.

Ukiachia mbali umiliki wa studio yake ya Mwanalizombe, Jay amewekeza kwenye biashara mbalimbali ikiwemo saluni ya kisasa iliyopo Msasani na shule ya watoto iliyopo jijini Dar. Pamoja na ubunge, Jay ameendelea kufanya muziki kwa kutoa ngoma kali zinazomuingizia mkwanja kupitia YouTube na shoo mbalimbali.

Kwa utajiri alionao, ukiacha ule mjengo wake uliobomolewa ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro pale Kimara- Temboni jijini Dar, jamaa huyu anamiliki mjengo mwingine na viwanja jijini Dar na jimboni kwake, Mikumi mkoani Morogoro. Baada ya ubunge, sasa Jay anasukuma ndinga kali aina ya Toyota Land Cruiser V8 na magari mengine ya kawaida.

VICK KAMATA LIKWELILE

“WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele… yelele…” Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), mkoani Geita, Vicky Kamata ni mwanamuziki ambaye muziki umemfanya afahamike na anayetajwa kuwa na utajiri balaa.

Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni. Vicky ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.

“Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky.

Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita. Ana nyumba ya ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam anamiliki magari manne ya kifahari, ana Toyota Voxy, BMW X5, na Toyota Land Cruiser ‘VX’ ma ana gari aina ya Toyota Altezza.

Wanamuziki hao wamefanya wasanii wengi kutaka kuingia kwenye siasa, kwa kuwa muda unakaribia wa kusaka wabunge na madiwani, tusubiri tuone.

BABU TALE

Huyu ni meneja wa mwanamuziki Diamond ambaye amewania kupitishwa na CCM kuwa mgombea ubunge jimbo la Morogoro Kaskazini na kushinda katika mchakato wa kwanza wa kura za maoni.

Ni wazi kwamba kutokana na kupendwa muziki wa anayemmeneji, babu Tale amejizolea umaarufu kwa wanachama wa chama tawala na kufanikiwa kuwashinda wenzake katika kura za maoni.

Babu Tale kuongoza wanamuziki kumefanyaka kuwa na maendeleo ya kiuchumi.


ABASS TARIMBA

Kama ilivyo kwa Babu Tale, Abbas Tarimba naye kupitia michezo na burudani kumemfanya ajulikane zaidi na alipoamua kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni ikawa kazi rahisi kwake kutambuliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Kinondoni, hivyo kushinda katika mchakato wa kura za maoni.

Tarimba ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni maarufu ya michezo ya SportPesa inayodhamini mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.

MAKALA: ELVAN STAMBULI
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger