8/15/2020

UN yaangusha azimio la Marekani kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya IranBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeliangusha kwa kishindo azimio la Marekani la kurefusha kwa muda usiojulikana vikwazo vya Umoja wa Mataifa vya silaha dhidi ya Iran.

Serikali ya Trump imepata tu uungwaji mkono kutoka kwa Jamhuri ya Dominika pekee lakini imeapa kuchukua hatua zaidi ili kuizuia Iran kuuza silaha.

Azimio hilo lilipata kura mbili za kuunga mkono na mbili za kupinga.

Wanachama 11 hawakushiriki na kuliacha azimio hilo bila ya kura tisa za "ndiyo" zinazohitajika ili kuidhinishwa. Urusi na China zilipinga vikali azimio hilo lakini hazikuhitaji kuzitumia kura zao za turufu.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema kushindwa kwa Baraza la Usalama kuchukua hatua ya kulinda amani na usalama wa kimataifa haikubaliki.

Marufuku ya biashara ya silaha inamalizika Oktoba 18 chini ya masharti ya azimio ambalo liliwezesha makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyotiwa saini Julai 2015
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger