8/01/2020

Usibadilike Temporarily Kwa Sababu Unataka Uonekane Wife/Husband Material ili Umu Impress Mtu


Usibadilike TEMPORARILY kwa sababu unataka uonekane Wife/Husband Material ili umu-impress mtu halafu mkifika ndani unarudia rangi-rangi zako zilezile ambazo ndio NATURAL YOU
Muache akupende kwa Ulevi wako,Kwa Umbea wako,Kwa Kutoa kwako udenda ukilala,Kwa kuwa mchafu na kutofua Boxer,Kwa kunuka kikwapa cha njano,Kwa Umaharage ya Mbeya wako, Kwa sababu kama akikupenda KAMA ULIVYO LEO hata mkiingia ndani ATAKUPENDA TU kwa sababu alijua aina ya mtu anayeingia naye ndoani na ameshajipanga kisaikolojia kuvumilia harufu ha Boxer zako...

Ukimuimpress kwamba hunywi kwa miezi mi3 akakuoa halafu HAMAD anakuta chupa za Ndovu stoo PATACHIMBIKA

Zimwi likujualo halikuli likakwisha,Muonyeshe rangi zako halisi akupende kwa Uhalisi wako lasivyo utaolewa leo SAWA na bajeti ya milioni 96 lakini Jiandae kuwa mjane baada ya Miezi 6 kwa karatasi ya Talaka ya Sh 50 Steshenari.
BE YOURSELF.
By Seth
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger