Viongozi wa Afrika Magharibi walitaka jeshi la Mali kumuachia huru Rais Keita

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Viongozi wa Afrika Magharibi wameongeza shinikizo dhidi ya kundi la wanajeshi waliotwaa madaraka nchini Mali kwa sasa wakilitaka jeshi hilo limuachie Rais Ibrahim Boubacar Keita na kumkubalia arudi mamlakani.

Haya yanajiri siku chache baada ya kiongozi huyo kulazimishwa kujiuzulu na wanajeshi hao waliompindua.

 Viongozi wa mataifa ya Shirika la mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS pia wametaka kuweko na jeshi la kando wakisema Keita anastahili kukubaliwa aendelee kuongoza katika miaka yake mitatu iliyosalia.

Keita mwenye umri wa miaka 75 pamoja na waziri wake mkuu bado wamezuiliwa na jeshi hilo katika kambi ya jeshi ya Kati.

ECOWAS imesema jeshi hilo ndilo lililo na dhamana ya usalama wa Keita na maafisa wengine wa serikali wanaozuiliwa.

Umoja wa Mataifa na Ufaransa wametaka hali ya utulivu na kuheshimiwa kwa sheria nchini Mali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad