8/09/2020

Wafahamu Wateule wa Rais Magufuli Hii Leo


Rais Magufuli amemteua Ngw'ilabuzu Ludigija kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala akichukua nafasi ya Mussa Chogelo ambaye amepangiwa kazi nyingine kwenye ofisi ya Rais, kabla ya uteuzi huo Ludigija alikuwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.


Uteuzi huo umefanyika hii leo Agosti 9, 2020, na tarifa hiyo kutolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo pia Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi Erasto Kiwale, ambaye atakwenda kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.

Aidha Rais Magufuli amemteua Catherine Mashalla kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, ambapo kabla ya nafasi hiyo alikuwa ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Kigamboni, ambapo uteuzi pamoja na uhamisho wa viongozi hao unaanza leo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger