8/18/2020

Wafungwa 11 Watoroka Seli Baada ya Kuchimbia Shimo Ukutani, Mmoja Apigwa Risasi


Mmoja wao alipigwa risasi mguuni alipokuwa akitoroka na kukamatwa tena. Picha: Hisani

Wafungwa wao waliokuwa wametiwa rumande kwa makosa mbali mbali walitorokea shimo hilo na kuwaacha wenzao

Polisi walijuzwa kuhusu kisa hicho na wafungwa waliosalia ndani

Mmoja wao alipigwa risasi mguuni alipokuwa akitoroka na kukamatwa tena

Zaidi ya wafungwa 11 wametoroka katika seli ya kituo cha polisi cha Bungoma walikozuiliwa.

Maafisa wa polisi wanaochunga seli hiyo walipata habari kuhusu kisa hicho mwendo wa 3am baada ya kupashwa habari na wafungwa waliosalia humo.

Kulingana na runinga ya Citizen, wafungwa hao walitoroka baada ya kuchimbia shimo katika ukuta wa seli hiyo.

‘’Wafungwa hao walikata chuma cha mlango wa seli na kutumia katika kuchimba shimo ukutani,’’ ripoti ya Citizen.


Wafungwa hao walitoroka baada ya kuchimbia shimo katika ukuta wa seli hiyo. Picha: Hisani.

Maafisa wa polisi walianza msako dhidi ya wafungwa hao waliotoroka na kumpata mmoja aliyetambulika kama Isaac Wekesa akikimbia kuingia msituni karibu na uwanja wa ndege.

Wekesa alipigwa risasi pajani kabla kukamatwa tena na kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma  kwa matibabu.

Wafungwa hao waliotoweka wametambulika kama Brian Ochieng Onyango, John Wanyonyi , Clerkson Otieno, Simon Wekesa na Collins Juma Nyukuri.

Wengine ni Alex Simiyu Muyekho, Bramwel Barasa, Pascal Kiberenge Namasaka, Emmanuel Wakoko na John Barasa Wekesa.

Polisi sasa wameanzisha msako mkali dhidi ya wafungwa hao waliotoroka ili kuhakikisha kuwa wanachukuliwa hatua za kisheria.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger