8/23/2020

Wahamiaji Haramu 51 Wakamatwa Eneo La Msata Mkoani PwaniJESHI la polisi mkoani Pwani ,linawashikilia wahamiaji haramu (wanaume ) ,kutoka nchini Ethiopia wapatao 51,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .


Kamanda wa polisi mkoani humo,Wankyo Nyigesa alithibitisha juu ya tukio hilo ambapo alisema ,huko eneo la Mzani wa magari Msata ,Chalinze ,polisi wakiwa doria barabara kuu ya Chalinze kuelekea Tanga ,lilikamata gari namba T.246 BBG aina ya scania tani 10 ,hard top .


Alieleza ,gari hilo lilipopekuliwa lilikutwa likiwa na raia 51 wote wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 15-25 ambao walikuwa wanasafirishwa kutoka Tanga -kuelekea Chalinze kupitia Msata na watu wawili wanaodhaniwa kuwa waTanzania ambao walitoka ndani ya gari na kukimbia .


Wankyo alibainisha gari hilo linaonyesha linamililiwa na Uswege Mwamboma ,wa Tukuyu Mbeya .


Kamanda huyo aliwataka mmiliki wa gari na ambao wamehusika kuwasafirisha wahamiaji hao haramu kujisalimisha wenyewe kabla hawajatiwa nguvuni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger