Wanaanga Wawili wa NASA Watua Salama Duniani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wanaanga wawili wa Marekani wamerejea salama kwenye sayari ya dunia kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga, wakihitimisha hatua ya kihistoria ya majaribio ya safari za binaadamu kuelekea anga za juu kwa chombo cha SpaceX.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanaanga wa Shirika la Anga za Juu la Marekani, NASA, kutuwa kwenye maji tangu mwaka 1975, na pia mara ya kwanza kwa kampuni binafsi, na sio NASA, kusafirisha watu kwenda na kuwarudisha kutoka mstatili wa dunia.

Bob Behnken na Doug Hurley, walioongoza chombo cha SpaceX Crew Dragon, walituwa kwenye Ghuba ya Mexico kando ya pwani ya Florida jana, Jumapili.

Wanaanga hao walianza safari yao huko huko Florida mwezi Mei mwaka huu.

Kwa kampuni ya SpaceX inayomilikiwa na bilionea Elon Musk, safari hii lilikuwa jaribio la mwisho lililohitajika kabla ya NASA kuipatia cheti cha kusafirisha watu, hatua ambayo inaweza kufunguwa njia kwa utalii wa anga za juu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad