Wanandoa waliodumu kwa miaka 79 watuzwa na Guiness

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wenza hawa walioana mwaka 1941, kwa ndo aya siri baada ya familia zao kutoidhinisha mahusiano yao. Bwana ana miaka 110 na bibi miaka 104.


Ndoa yao, iliyoanza kwa siri imedumu kwa miaka 79 na wenza hawa kwa pamoja wameishi si chini ya miaka 215 kwa ujumla.


Julio Mora na Waldramina Quinteros wamekuwa pamoja kwa muda mrefu kuliko wenza wengine wengi walio hai.


Bwana mwenye miaka 110 na bibi 104 wametambulika kuweka rekodi ya dunia ya Guiness kwa wenza walio na umri mrefu zaidi duniani.


Wapenzi hao raia wa Ecuador ,Mora alizaliwa tarehe 10 mwezi Machi , mwaka 1910 na Bibi Quinteros tarehe 16 mwezi Oktoba mwaka 1915.


Kuna ndoa zenye umri mrefu ambazo Guiness inazitambua, lakini hakuna yenye wenza walio na umri mkubwa zaidi


Wapenzi hawa walioana mwaka 1942 katika kanisa la kwanza kujengwa mjini Quito, Uhispania: La Iglesia de El Belen. Julio aliwakimbia wazazi wake na kwenda kumuoa mpenzi wake baada ya kutopata ridhaa ya familia.


''Hatukuachana,'' alisema Bi Quinteros.


Wote walimu ambao wamestaafu na wanaishi eneo katikati ya mji wa Quito, mji mkuu wa Ecuador.


Kwa pamoja wanaweza kukusanya watu wengi kutokana na uzao wao: wana watoto wanne walio hai, wajukuu 11, vitukuu 21 na kilembwe kimoja.


Mwanzoni mwa mwaka, mmoja wa wajukuu wao alisema kuwa wazee hao huenda wakawa miongoni mwa wenza walio na umri mkubwa duniani.


Mtoto wao Cecilia kisha akatuma nyaraka kwa Guiness kisha wakapata uthibitisha katikati ya mwezi Agosti.


Wote wako timamu na wenye afya njema, Cecilia anesema, ingawa afya yao ya akili ilitikiswa kutokana na janga la corona.


''Kwa mwezi mmoja wamekuwa tofauti, wamekuwa wenye huzuni, kwa kuwa wanakosa mikusanyiko ya familia,'' alisema.


Tangu mwezi Machi, hatujakutana hata mara moja. Wazazi wangu wanahitaji kuwa na familia.''


Cecilia amesema wenza hao wanapenda kwenda kwenye jumba la sinema na maonesho wakiwa pamoja. Anasema baba yake anafurahi sana kutazama runinga na kunywa maziwa. Mama yake, anapenda kitinda mlo (desserts) kusoma magazeti kila asubuhi.


Alipoulizwa kama ana ushauri kwa wale wanaotamani kuishi maisha marefu, Bi Quinteros amesema: ''ninashauri kusema kweli. Usiseme uongo, uongo unaweza kuipoteza dunia.''


Awali waliokuwa wanashikilia rekodi ya kuwa wenza wenye umri mrefu walikuwa wakazi wa Texas Charlotte na John Henderson, ambao kwa pamoja walikuwa na jumla ya miaka 212 na siku 52.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad