8/31/2020

"Wanasambaza eti Konde ameanguka na kamba wanaona donge hao" HarmonizeSuala ambalo lipo trending kwa sasa mitandaoni na midomoni mwa wapenzi wa burudani ni kuhusu tuhuma za kuanguka kwenye kamba kwa msanii Harmonize wakati anafanya show siku ya Wananchi ya Uwanja wa Benjamin William Mkapa.


Baada ya tukio hilo kutokea limegusa hisia za watu wengi na kila mtu kusema lake ambapo yeye mwenyewe ametumia 'freestyle' na kuachia mistari ambayo inalenga  kuwachana wale wote waliomdiss baada ya kuanguka kwake.


"Wanasambaza eti Konde ameanguka kamba haishukwi kama baiskeli, wanaona donge hao wanyonge, tunavyoua kwenye show wao wanaona donge, Konde akishuka na kamba wanaona donge hao"


Baadhi ya wasanii wengine waliofanya show kwenye kilele cha siku ya Wananchi kwa timu ya Yanga ni Madee, Maarifa, Billnass, G Nako , Shilole, Baba Levo na Mzee wa Bwax.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger