8/09/2020

Wanasimba mtulie, Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja, tuko Imara – Mo DewjiMwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji amewataka Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa soka kutulia na kuwakumbusha kuwa wametoka mbali na wameyapitia mengi.

Mo ameandika ujumbe huo muda mchache tu baada ya Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa kutangaza kujiuzulu na kuwepo na tetesi kuhamia upande wa pili kwa hasimu wao Yanga SC.

‘Tumetoka mbali na bado safari inaendelea; tumepita mengi Wanasimba wenzangu. Nawaomba Wanasimba wote mtulie. SIMBA SC ni kubwa kuliko mtu moja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali SIMBA. Kazi inaendelea, tuko IMARA!,” – Mo Dewji

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger