8/17/2020

Watu wa Kariakoo Sio Wazuri Hata KIDOGO...Ona Walichomfanyia Tshishimbi Mpaka Akajikuta Hana Timu ya Kumsajili....

Watu wa Kariakoo wahuni sana, muulize Tshishimbi. Walianza Simba kwanza. Wakamjaza kama wanamtaka na yeye akajaa akaanza kudengua Jangwani. Watu wa Jangwani wakamjaza kama wanapambana kumbakisha na wakampatia pesa. Baadae wakageuza mawazo kimya kimya. Akagoma kusaini ingawa alikuwa na pesa zao. Wakamwambia arudishe wataongea upya kumbe wanajua ana tatizo kubwa la goti. Akarudisha pesa wakazichukua wameenda Congo kumchukua Tanombe Mukoko ambaye ni bora kuliko yeye.

Huku Simba alikotegemea wangemfukuzia wakamkalia kimyaaaa. Unamchukua Tshishimbi wa nini wakati una Fraga na Jonas ambao ni wamoto kweli kweli. Lakini Simba kwa jinsi wanavyojisikia hivi wanawezaje kumchukua mchezaji aliyetangazwa kuachwa Yanga?

Hatimaye akabaki hana pakwenda. Majuzi nasikia kapanda Ethiopian Airline kurudi kwao...hana hamu na wahuni wa kariakoo...sio watu wale. Pepo wataisikia tu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger