8/24/2020WAZIRI wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harisson Mwakyembe amesema kuwa Klabu ya Azam FC imeongeza thamani ya soka nchini na kujitengenezea nafasi ya kuwa timu kubwa na bora nchini.

Maneno hayo aliyasema jana Agosti 23, kwenye kilele cha Azam Festival makao makuu ya Azam FC, Chamazi.


Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa na udhuru.


"Serikali ambapo huwa inakwama kwenye masuala ya kimichezo ikiwa ni pamoja na uwanja huwa inakimbilia huku kwa Azam kwa kuwa mmejipambanua na kuwa bora katika miundombinu pamoja na kuwa na timu bora.


"Pia ni timu ambayo ina academy yake pamoja na miundombinu bora, kwa tamasha ambalo mmelifanya limeongeza thamani ya timu yenu na ninaamini kuwa mtazidi kuwa bora," amesema.


Burudani zilitolewa kwa mashabiki jana ikiwa ni pamoja na mechi za utangulizi, show kali kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba pamoja na msanii wa Singeli, Msaga Sumu.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger