8/14/2020

Willian Da Silva ni mali ya Arsenal


Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa aliyekua mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea, Willian da Silva kwa mkataba wa miaka mitatu.


Winga, Willian da Silva (Kulia Pichani), akisaini mkataba wa kuitumikia Arsenal akiwa na Kocha wake wa sasa Mikel Arteta (Kushoto Pichani) .

Mkataba wa nyota huyo wa kibrazil na Chelsea ulimalizika lakini pande hizo mbili hazikufikia makubaliano ya kuongeza mpya ambao unadaiwa haukua na maslahi mazuri kwa mchezaji.

Inadaiwa kuwa Chelsea ilimpa mkataba wa miaka miwili nyota huyo wa Brazil wenye thamani ya mshahara wa paundi laki moja kwa wiki, lakini Arsenal wamempatia mshahara wa paundi laki mbili na ishirini kwa wiki.

Willian alijiunga na Chelsea mwaka 2013 akitokea Anzhi Makhachakala ya Urusi kwa dau la paundi milioni 30 na ameichezea jumla ya michezo 339.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger