8/18/2020

Yanga Wamzimia Simu Beki MnyarwandaHALI imeenda ndivyo sivyo katika usajili wa Eric Rutanga baada ya beki huyo kusema kuwa mabosi wa Yanga wamemchunia tangu asaini mkataba wa awali na timu hiyo.

Rutanga ambaye hapo awali alituthibitishia kuwa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambapo alikuwa akisubiri kutumiwa tiketi ili kuweza kuwasili nchini.

Akizungumza na Championi Jumamosi,beki huyo alisema kuwa tayari alishasaini mkataba wa miaka miwili wa kukitumikia Yanga na baada ya hapo viongozi walimwambia atulie mipaka ikifunguliwa atatumiwa tiketi ya ndege jambo ambalo limekuwa tofauti mpaka sasa.

“Nilisaini mkataba na Yanga wa miaka miwili baada ya hapo viongozi wa Yanga waliniambia kuwa nisubiri mipaka ya Rwanda itakapofunguliwa lakini nashangaa hali imekuwa tofauti mpaka sasa.

“Nimekuwa nikiwatumia meseji lakini imekuwa kimya na hawajibu kabisa, hivyo nimekuwa na wasiwasi na dili hili ambalo nilikuwa nina uhakika nalo,” alisema beki huyo.

Dili la Rutanga na Yanga linaweza likaota mbawa kutokana na Yanga kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Polisi Tanzania, Yassin Mustapha.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger