8/14/2020

Zari Amkata Maini Mobeto


MWANAMAMA mjasiriamali na mzazi mwenzake na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amemkata maini mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye alitikisa na bethidei ya mwanaye.

Iko hivi; awali Mobeto alianza kutikisa mitandao kwa kuposti picha kali za mwanaye Dyllan aliyezaa na Mondi na kutikisa kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram.

Pongezi zilikuwa kama zote, huku watu wakimsifia Mobeto kuwa ndiye anayefaa kuolewa na Mondi ambaye ametangaza kufunga ndoa Oktoba 2, mwaka huu.

Kama hiyo haitoshi, bethidei hiyo iliongezewa kiki zaidi na Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi ‘Jaguar’ ambaye alimposti mwanaye huyo na kuzua gumzo kama lote. Wafuasi mbalimbali walipongeza muonekano wa mtoto huyo na kumsifia Mobeto kwa kuzaa kidume cha nguvu.

Ghafla ‘bin vuu’, Zari akaibuka na picha kali za mwanaye Tiffah aliyezaa na Mondi na kusababisha watu waache kujadili tena zile za mtoto wa Mobeto.


Zari aliposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram, ikionyesha sherehe hiyo ambayo ilifanyika mjini Durban, Afrika Kusini ambako anaishi na watoto wake.

“Mhhh Zari ni kiboko yao, yaani kajua kupangilia maana kamfanyia sherehe mtoto wake kama harusi vile, yote ni kumkomoa ‘mke’ mwenziye Hamisa, maana yeye kaposti mipicha tu, ila Zari kajibu kisomi,’’ aliandika shabiki mmoja.
 
Wakati yote hayo yakiendelea, mama mzazi wa Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’, alionesha mapenzi ya dhati kwa kumposti sana na kumsifia Tiffah ambaye ni mjukuu wake, kitu ambacho kilimpaisha zaidi mtoto wa Zari.

“Kiboko ya Naseeb kichwa Latipha, pacha wa Bi Sandra,’’ aliandika Mama Dangote.

Tiffah ambaye amezaliwa Agosti 6, mwaka 2015 alikuwa akitimiza umri wa miaka mitano. Ni mtoto wa kwanza wa Mondi na mtoto wa nne na wa kike pekee wa Zari.


Naye Dyllan ambaye ni mtoto wa pili wa Hamisa, alikuwa akitimiza umri wa miaka mitatu.


Bifu la Zari na Hamisa, lilianza mwaka 2015 pale ambapo Zari alipata taarifa kuwa Hamisa anatembea na Mondi, ambapo baadaye bibie huyo wa Kiganda alitangaza kuachana na Mondi huku Mobeto naye pia akiachana na staa huyo.

Happyness Masunga, Risasi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger