8/14/2020

Zari ‘Boss Lady’ Atunukiwa Tuzo za 'One Africa'Mfanyabiashara na nyota wa mtandaoni ‘socialite’ kutoka Uganda, Zari ‘Boss Lady’ Hassan ndiye mshindi wa mwaka huu wa tuzo za 'One Africa'.


Zari ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini alitangazwa mshindi wa kitengo cha 'Mitandao ya kijamii', katika tuzo hizo ambazo zinawatambua waafrika walio na mchango mkubwa katika ukuzi wa jamii.Hata hivyo, kutokana na janga la Corona, tuzo za mwaka huu hazikuandaliwa kama ilivyo kawaida, japo washindi walitangazwa mtandaoni.Zari, aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Flava Diamond Platnumz, aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram na kushukuru One Africa kwa tuzo hiyo, ambayo anasema ni kutokana na juhudi zake katika fani ya muziki na biashara.Wakati One Africa ikimtangaza Zari kama mshindi, ilisifu ari yake katika kuhakikisha ufanisi wa muziki na maendeleo ya kijamii.“Bidii yake ya kutaka mafanikio na kutimiza ndoto zake ni ya kutia moyo sana na imewachochea wengi barani Afrika...” ilisema taarifa ya timu ya Tuzo za One Africa.Zari alitangazwa kuwa mshindi pamoja na bingwa wa muziki wa Afrika Burna Boy aliyeshinda kitengo cha 'Muuzaji bora wa utamaduni mwaka 2020'.Burna Boy, ambaye majina yake kamili ni Damini Ebunoluwa Ogulu Rex, ni mwanamuziki kutoka Nigeria aliyepata sifa kubwa kwa kupeperusha bendera ya Afrika duniani kote kupitia muziki wake.Tuzo za One Africa zinasherehekea juhudi za bara Afrika katika kuafikia Malengo Endelevu, yaani 'Sustainable Development Goals (SDGs),' ambayo ni miradi ya kuboresha maisha ya siku za baadae.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger