Zijue Aina za Mbwa 20 Hatari zaidi Duniani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Habarini za Alhamis natumaini mpo salama sana. Naomba kuleta Uzi huu maalumu kuhusu tunaopenda kufuga mbwa. Duniani kuna aina nyingi sana za breed ya mbwa achilia mbali German Sheepshead na Bull Dog au Chihuahua. Kuna breed hatari sana zaidi ambazo zinaweza kuleta shida kwa mfugaji wake.
Hapa ninaweka breed 20 ambazo lazima ukae chonjo ukiwa nazo.

10. Inu.
Huyu ni mbwa ama breed ya mbwa yenye uzito kuanzia kilogramu 58 mpaka kilogramu 90. Na ana urefu unaoanzia inch 24 mpaka 32. Kiuhalisia huyu ni mbwa Wa mapambano na baadhi ya nchi wamekata kufuga mbwa Hawa kabsa. Mfano mzuri sana ni Inu aina ya Shiba anayepatikana katika nchi ya Japani, ambaye huyu hutumika kwenye kuwinda. Pamoja na aina nyingine Tosa Inu.

9. American Bandogge.
Huyu ni cross breed ya American Pit bull Terrier pamoja na Neapolitan Mastiff. Sasa huyu Pit bull Terrier ni mkorofi balaa unakwenda kuchanganya na kiburi cha Neapolitan Mastiff. Hapo unakwenda kutengeneza mbwa mmoja mkatili sana.
Ni mbwa aliyejaa misuli sana, ijapokuwa alipofanyiwa breed hakukuwa na malengo ya kuwa mbwa Wa kupigana lakini matokeo yake yakawa ndo hivyo.

8. Cane Corso.
Mbwa kwenye uzito kuanzia kilogramu 44 mpaka 68. Kuanzia sura mbaya mpaka tabia yake hakika ni mbwa mwenye ukali Wa kipekee. Akiwa ni breed ya Mbwa aina ya Canis Pugnax ambao Hawa ni mbwa waliotumika na Warumi kwenye Vita. Hivyo damu inatembea ndani ya Cane Corso.

7. Bull Terrier.
Mbwa hawa wana kichwa kikubwa lakini wanaongoza kwa kuwa na misuli mikubwa na imara sana. Ana uwezo Wa kuwinda kwa ukali na ukatili sana hasa hasa kwa wanyama wadogo.

6. Dogo Argentino.
Huyu ni mbwa mrefu,mkubwa na aliyejaa misuli sana, chimbuko lake ni Argentina kwa lengo la kusaidia kuwinda. Na inasemekana alifanyiwa breed ili kuweza kupambana na wanyama kama Puma pamoja na Dubu mwitu.

5. Boer Boel.
Mbwa mkubwa sana na ni breed ya Mastiff kutoka kwenye South Africa. Alifanyiwa breed kwa lengo la kulinda mashamba au nyumbani. Mwanzoni walitumika kama mstari Wa mbele kupambana na mbwa mwitu. Pia hata kwenye mawindo ya mwituni mfano nyati au swala walikuwa na uwezo Wa kufuatilia mnyama na kumchukua mpaka kwa mwenye naye. Ni mbwa wenye uaminifu sana nyumbani pia kulinda familia zao.

4. Gull Dong.
Anajulikana sana kama (Pakistan Bull Dog) akiwa ni cross breed ya Gull Tarrier pamoja na Bully Kutta. Ana nguvu sana na alifanyiwa breed kama mbwa mpiganaji. Ni ngumu sana kumtunza na ana hasira za karibu.

3. American Bull Dog.
Huyu ni mbwa mwenye misuli mingi kuzidi mbwa wote. Ukisikia inafika sehemu mtu anampiga shaba mbwa wake basi jua kuwa American Bull Dog ni moja wapo. Kwani wana tabia ya kuwa wagumu kusikia na kufuata maagizo. Alifanyiwa breed kwa lengo la kupambana na dubu mwitu, pamoja na kulinda mifugo ikiwemo na mali.

2. Wolf Hybrid.
Kama jina linavyosema hapo, huyu ni mbwa mwenye breed ya mbwa pamoja na Mbwa mwitu. Huyu alifanyiwa breed na kupelekea kuwa na tabia zinazoshabiana na Mbwa mwitu. Hana tabia inayoeleweka kwani anaweza kuwa kama mbwa lakini baadaye anakuwa kama mbwa mwitu tena.

1. Rottweiler.
Huyu naomba nimuweke namba moja maana ni mbwa mwenye kiburi balaa kwank ni breed ya American Bull Dog pamoja na Mbwa mwitu. Na anaanza kubadilika tabia akiwa na miaka 3 tu.

Bonus:
1. German Shepherd.
Huyu nimemweka bonus. Ni mbwa mwenye akili sana, anajiamini sana, sio muoga na anapendwa kutumiwa na Polisi kwenye kutuliza ghasifa. Lakini cha ajabau ni kuwa jike hawezi kuvumilia ukicheza na Watoto wake kwani anaweza kukushambulia mpaka kifo.

2. Pitbull.
Hili ni jina linalotumika kuelezea breeds za mbwa kama vile: American Pit bull Terrier, the Staffordshire bull Terrier, the American Staffordshire Terrier and the American Bull Dog. Huyu ni mbwa mahususi kuwinda na kuzuia dubu pamoja na Ngombe mwitu. Pia Pitbull walitumika kupiganisha mbwa na ni kati ya mbwa wenye hatari kubwa duniani.

3. Causanian Ovcharka.
Anajulikana kama Caucasian Shepherd na lengo kubwa ilikuwa ni kutengeneza breed ya mbwa atakayelinda mifugo. Lakini mbwa huyu ni mkali na hatari hasa kwa watu asiowatambua kabsa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad