Zitto Zuberi Kabwe: Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo na kila Kata

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ametoa wito kwa vyama vya upinzani nchini kuwa viache ubinafsi kwa kuwa Tanzania ni kubwa kuliko vyama na kwamba Watanzania hawatowasamehe kama hawatoamua kuwa na mgombea mmoja wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 18, 2020, Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mpaka sasa viongozi wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya vyama hivyo kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao na anaamini kuwa Watanzania wengi wanataka mashirikiano.

Watanzania hawatatusamehe tusipokuwa na mgombea mmoja wa Urais, mgombea mmoja kila Jimbo,na kila Kata, wito wangu kwa viongozi wenzangu wa vyama vya upinzani tuache ubinafsi, Watanzania wanataka ushirikiano ili kuleta mabadiliko katika nchi, na joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka Bara na Visiwani" amesema Zitto Kabwe.

Zitto ameongeza kuwa yeye na chama chake wako tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuweza kuitoa CCM madarakani.

Chanzo: EATV
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad