9/22/2020

ACT-Wazalendo yaungana na CHADEMA

 


Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo taifa, Maalim Seif Sharrif Hamad amemuidhinisha  mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwa na Aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Bernard Membe.


Akizungumzia hatua hiyo, Naibu Katibu wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Janeth Rite amesema kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa katika mkutano wake wa kampeni katika Jimbo la Donge aliweka wazi suala hilo.


"Saa chache zilizopita, Mwenyekiti wa Kitaifa wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad amemuidhinisha Tundu Lissu na hayo ni matokeo ya mazungumzo ya chini chini yaliyokuwepo kati yetu na CHADEMA, hivyo hayo ndiyo maridhiano yetu", amesema Janeth.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger