9/18/2020

Alcantara kutua Liverpool kwa dau la bilioni 74

 


Klabu ya Liverpool inakaribia kukamilisha usajili wa kiungo Thiago Alcantara  kutoka Bayern Munich ya Ujerumani kwa ada ya uhamisho ya fedha za Uingereza pauni milion 25 ambayo ni zaidi ya bilioni 74 kwa pesa za kitanzania.

  

Kiungo huyo raia wa Hispania amekuwa akihusishwa kujiunga na Liverpool toka mwezi julai baada ya kuweka wazi kuwa hata saini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia the Bavarians pindi mkataba wake utakapo malizika mwishoni mwa msimu huu.

 

Hivyo Bayern wamefikia uamuzi wa kumuuza katika dirisha hili la kiangazi kwani endapo kama wangemuacha aondoke mwishoni mwa msimu huu wasingepata chochote angeondoka akiwa mchezaji huru.


Katika uthibitisho kuwa kiungo huyo anaondoka asubuhi ya Leo Mwenyekiti wa Bayern Minich Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kuwa klabu yao imefikia makubaliano na Liverpool na Thiago anaondoka.

'FC Bayern imefikia makubaliano na Liverpool, Thiago anaondoka' amesema Karl-Heinz Rummenigge

Liverpool italipa kwanza ada ya uhamisho ya pauni milion 25 ambayo ni zaidi ya bilion 74 kwa pesa za kitanzana na wataongeza pauni milion 5 ambayo ni zaidi ya bilion 14 kwa pesa za kitanzania endapo kama kikosi cha Liverpool kitashinda ubingwa wa klabu bingwa ulaya au ubingwa wa ligi kuu England EPL.

Alcantara mwenye umri wa miaka 29 ameshafanya mazungumzo binafsi na liverpool atasaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Liverpool na atavaa jezi namba sita, kilichobaki ni kufanya vipimo vya afya kabla ya kutangwa kuwa mchezaji rasmi wa Liverpool.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger