Aliyefungwa Jela Akiwa na Miaka 18 Aachiwa Akiwa na Miaka 100

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPABabu mwenye umri wa miaka 100 aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la mauaji nchini Nigeria ameachiwa huru kwa msamaha wa Serikali.

Celestine Egbunuche ametumikia miaka 18 jela hadi wiki hii, baada ya kukutwa na hatia ya kupanga mauaji.


Baada ya kuachiwa huru, alikutana na familia yake nje ya gereza la Enugu ambalo lina ulinzi mkali zaidi. Mwanaye, Chisom Celestine alieleza jinsi alivyofurahi kumuona tena baba yake uraiani.

“Nilifurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa siku hii. Mimi ni mtu mwenye furaha zaidi duniani sasa hivi,” alisema.

Egbunuche ambaye hivi sasa anasumbuliwa na magonjwa kama kisukari na matatizo ya kuona, amewekwa chini ya uangalizi wa kimatibabu hospitalini.

Hata hivyo, mwanaye amesema kuwa hana uwezo wa kifedha wa kumsaidia baba yake kupata matibabu.

Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imeendelea kufanya kampeni kutafuta namna ya kumsaidia.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad