Askari 9 wameuawa na wanamgambo wa kundi la Boko haramu nchini NigeriaWanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haramu  wamewavamia  askari wa jeshi la Nigeria na kusababisha vifo vya watu   askari 9  Kaskazini-Mashariki  mwa Nigeria. 


Wanamgambo wa kundi la Boko Haramu wamevamia  kambi ya Magumeri Borno  na kupelekea vifo hivyo. 


Vyombo vya habari  katika eneo hilo  zimefahamisha kuwa  kambi ilioashambuliwa  sio mara ya kwanza  kushambuliwa na  wanamgambo wa  Boko haramu. 


Katika shambulizi hilo, magairi  matatu ya jeshi  wameteketezwa kwa moto. 


Baada ya tukio hilo, jeshi la Nigeria limeendssha operesheni kali ambapo magaidi 20 wa kundi la Boko Haramu wameripotiwa kuangamizwa. 


Watu   zaidi ya  20 000 wamepoteza maisha  tangu mwaka 2009 katika mashambulizi ya  wanamgambo wa kundi la Boko Haramu.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments