ATCL Yarudisha Safari za Dar na Hahaya (Comoro) Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imerudisha safari za kawaida kati ya Dar es salaam (Tanzania) na Hahaya (Comoro) kuanzia 8/9/2020.

ATCL itafanya safari zake mara mbili kwa wiki, siku ya Jumanne na Jumapili. Abiria wote wanaotarajia kusafiri kwenda Comoro wanahitajika kuwa na cheti maalum kinachothibisha kuwa wamefanya vipimo vya COVID-19 na wajiandikishe katika ubalozi wa Comoro kabla hawajanunua tiketi.

ATCL wanawashukuru sana wateja wao kwa kundelea kuiamini Air Tanzania na kuendelea kutumia huduma zake popote pale tunaporuka.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments