9/07/2020

Baharia wa meli ya kubeba ndege ya Marekani atoweka Ghuba ya Arabuni
Jeshi la wanamaji la Marekani limeendesha zoezi la kumtafuta baharia aliyetoweka kutoka kwenye meli ya USS Nimitz wakati meli hiyo ilipokuwa kwenye shughuli ya doria katika eneo la kaskazini la bahari la ghuba ya Arabuni. Tukio hili limezuka wakati ikiwepo mivutano na Iran. 

Zoezi hilo limeendelea usiku kucha hadi leo Jumatatu. Msemaji wa jeshi la wanamaji la Marekani lililoko Bahrain, kamanda Rebecca Rebarich, amesema mabaharia waliokuwa ndani ya meli hiyo ya kubeba ndege walitoa tahadhari ya kutoweka kwa bahari huyo jana magharibi baada ya kumtafuta na kumkosa baharia huyo. 


Hata hivyo kamanda huyo amekataa kutaja jina la baharia huyo aliyetoweka akitoa sababu ya kutoruhusiwa katika sheria ya jeshi hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger