9/17/2020

Barbados yatangaza kumuondoa, Malkia Elizabeth kama kiongoziVisiwa vya Barbados vimetangaza nia yake ya kumuondoa Malkia Elizabeth kama kiongozi wa nchi hiyo na kuwa Jamuhuri.

”Muda umewadia wa kuachana na historia yetu ya kikoloni,” Serikali ya taifa hilo la kisiwa hicho cha Caribbean imesema.

Barbado ina lengo la kumaliza mchakato huo wakati wa kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wake kutoka Uingereza, itakayofanyika mwezi Novemba mwaka 2021.

Malkia alivyokutana na gavana general wa Barbados, Dame Sandra Mason katika kasiri la Buckingham mwaka 2018


Kasri la Buckingham lilisema kuwa ni suala la serikali na watu wa visiwa vya Barbados.


Chanzo cha habari katika kasri la Buckingham kimesema kuwa wazo hilo ”halikuja tu ghafla” na ” limekuwa likizungumzwa hadharani mara nyingi”, Mwanahabari wa BBC Jonny Dymond alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger