9/22/2020

Barbara wa Simba afanya makubaliano na timu ya AL Ahly ya MisriOfisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akiongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi wametembelea makao makuu ya klabu ya Al Ahly yaliyopo Jijini Cairo, Misri na kukubalina kushirikiana kwenye maeneo ya biashara, ufundi na uendelezaji wa wachezaji.

Pia wamekubaliana kujenga kituo cha kukuza vipaji kwa ushirikiano na timu ya Al Ahly ikiwa ni kituo cha kwanza nje ya Misri (barani ya Afrika) ambacho kitaendeshwa na Simba na klabu hiyo na hapo baadae timu hiyo kuja nchini kucheza mchezo wa kirafiki na Simba SC.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger