Bosi Simba Akutana na Rais wa CAF Cairo, Misri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez,  leo Septemba 24, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika, Ahmad Ahmad,  kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri.


Baada ya kukutana,  Ahmad amempongeza Barbara kwa kupata nafasi hiyo kubwa, lakini pia kumtaka kuitumia vyema ili kuonyesha kwamba anaimudu kazi hiyo ambapo itakuwa ni moja ya njia ya kuhamasisha wanawake wengine kushika nafasi za juu za uongozi wa soka.


 


Kwa upande wake Barbara amemshukuru Ahmad na CAF kwa mapokezi mazuri, lakini pia kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kukuza soka la Afrika.


Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa CAF, Abdelmounaïm Bah, Makamu Katibu Mkuu wa CAF, Anthony Baffoe na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad