Bwana Harusi Ajiteka Siku ya Harusi Kukwepa Kumuoa Mchumba Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Sherehe ya harusi ni siku ya furaha kwa wanaopania kufunga pingu za maisha, lakini hayo yalikuwa tofauti kwa jamaa moja ambaye aligeuza mtazamo wa hafla hiyo.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 55, kutoka nchini Colombia mji wa Pitalito, alikuwa anatazamiwa kula viapo vya ndoa na mchumba wake mbele ya jamaa na marafiki siku ya wikendi.

Bwana harusi ajiteka siku ya harusi nyara kukwepa kuoa mchumba wake
Jamaa alikuwa anapaniwa kula viapo vya ndoa na mpenziwe siku ya wikendi.
Huku terehe ya siku hiyo ikiendelea kukaribia, mwanamume huyo aliendelea kuingiza baridi na kukiri kwa baadhi ya marafiki zake kuwa anapania kuvunja harusi hiyo.

Bila ya kujua ya kufanya, swaiba zake waliwazia kughushi kuwa ametekwa nyara.

Bwana harusi ajiteka siku ya harusi nyara kukwepa kuoa mchumba wake
Bwana harusi alikuwa amewadikezea rafiki zake kuwa anapania kuvunja hafla hiyo.
Baada ya bibi harusi kuagizwa kujificha kwa siku kadhaa,rafiki zake walipiga ripoti kwa asasi za usalama huku wakidanganya namna walishuhudia akitekwa nyara na kundi la watu waliokuwa wamejihami.

Asasi za usalama zilichukua hatua ya haraka na hata kuwahusisha afisa wote wa polisi katika mkoa huo.

Hata hivyo, marafiki hao walijitokeza kukiri kwamba walidanganya ili kumsaidia mwenzao kuhepa kuhudhuria harusi yake.

Polisi waliamua kuficha jina la jamaa huyo ili kumlinda dhidi ya ghathabu za wakazi huku ikiripotiwa kuwa ni mara ya pili kwa jamaa huyo kuhepa kuhudhuria harusi yake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad