Cha mwisho alichokiona Bonge la Nyau kwenye ajali 'Lulu Diva Alianza Kulia Mama Nakufa'

 


Msanii Bonge la Nyau amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, ambapo amesema kitu cha mwisho walichokiona kabla ya kutokea kwa ajali ambayo wameipata siku zilizopita ni mwanga mkali mbele yao, kisha Lulu Diva akaanza kupiga kelele za "Mama Nakufaaa".


Bonge la Nyau amesema baada ya hapo waliona lori kubwa mbele yao ndipo dereva wao alipoamua kulitupa gari kwenye makorongo ili mradi wasigongane uso kwa uso maana ndiyo ingekuwa mbaya zaidi kwa upande wao.

"Lori na lori zilikuwa zinashindana kwenye ku-overtake kisha lori moja likaingia kwenye njia yetu, ghafla tukaona mwanga mkali sana kwenye gari letu, mara nikaanza kusikia kelele za Lulu Diva akisema "mama nakufa, mama nakufa",  dereva wetu alikuwa kwenye mwendo na ilikuwa usiku hivyo akalitupa gari kwenye korongo ili mradi tusigongane uso kwa uso maana ndiyo ingekuwa mbaya zaidi" ameeleza Bonge la Nyau

Bonge la Nyau, Lulu Diva na Belle 9 walipata ajali ya hiyo maeneo ya Chalinze wakati wanarejea Jijini Dar Es Salaam baada ya kutoka kwenye Kampeni za Chama cha Mapinduzi Kilolo Mkoani Iringa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

1 [disqus]: