Chanjo ya Covid-19, AstraZeneca yasitishwa, aliyefanyiwa majaribio aonesha dalili za ugonjwa usiofahamika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Majaribio ya kitabibu ya moja kati ya chanjo ambayo yamepiga hatua kubwa kupambana na ugonjwa wa COVID-19, inayotayarishwa na  kampuni ya madawa ya AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford, yamesitishwa kwa muda.


Hii ni baada ya  mtu aliyejitolea  kufanyiwa  majaribio kuanza kuonesha dalili za ugonjwa  ambao haufahamiki.


Wakati  mabilioni ya  watu duniani kote bado wanateseka  kutokana na  kuzuka  kwa  janga  hilo  la virusi  vya  corona  pamoja  na  idadi ya  vifo  duniani  kukaribia  laki 9, mbio duniani  kote kwa  ajili  ya kupatikana  chanjo  zinaendelea, ambapo  makampuni tisa  tayari yamo  mwishoni mwa  awamu ya  tatu  ya  majaribio.

Maambukizi duniani kote hadi sasa  ni  zaidi ya  watu milioni 27, na zaidi  ya  watu 890,000 wamefariki kutokana  na  ugonjwa  huo. Urusi tayari  imeidhinisha  chanjo , na  utafiti uliochapishwa  katika  jarida la  kitabibu la Lancet wiki iliyopita umesema  wagonjwa waliohusishwa  katika  majaribio ya mwanzo  walipata  chembe zinazokinga  mwili, na  hakuna  matatizo yaliyotokea. Lakini wanasayansi wanatahadharisha  kuwa  majaribio hayo  ni  madogo mno.


Msemaji wa  kampuni  ya  madawa  inayotengeneza  chanjo  hiyo AstraZeneca amesema  katika  taarifa  jana  kuwa  “tunasitisha  kwa hiari  chanjo  hiyo kuruhusu  hatua za  kuangaliwa  upya  data za usalama na  kamati  huru.


“Hii ni hatua ya kawaida  ambayo  inapaswa  kutokea  wakati  kuna uwezekano wa  ugonjwa  ambao  haufahamiki  katika  moja  kati ya majaribio, wakati  unachunguzwa, na  kuhakikisha  tunaendelea uhalali wa  majaribio.


Kampuni  hiyo  imesema  kuwa  katika  majaribio mengi, magonjwa baadhi  ya  nyakati yanatokea  kwa bahati lakini  ni  lazima kufanyiwa  uchunguzi huru.


AstraZeneca haikutoa  taarifa  zaidi, lakini  tovuti  ya  taarifa  za kitabibu  ya Stat News, ambayo  iliripoti kwanza  ugonjwa  wa  mtu huyo  aliyejitolea  kufanyiwa  majaribio, imenukuu  chanzo kikisema ugonjwa huo  umehusisha hali  mbaya ya mwili  kupambana  na chanjo  hiyo.


“Wakati bila  shaka  hizi si  habari  nzuri, kumbuka  kwamba uchunguzi  kamili  wa  hali  hiyo  ni  sehemu  ya  majaribio  ya kiwango  kikubwa na  muhimu  kuhakikisha  uaminifu katika  chanjo yoyote.


Hata  hivyo  itakuwa  na  maana  kwamba  matokeo yatacheleweshwa,”  mtaalamu  wa  magonjwa  ya  maambukizi kutoka  chuo  kikuu  cha  Harvard Bill Hanage aliandika  katika ukurasa wa  Twitter.


Kwa mujibu  wa  Stat News, mgonjwa  huyo aliyejitolea   kufanyiwa majaribio  ya  chanjo ana  uwezekano wa  kushiriki katika  awamu ya 2 na ya tatu  ya  majaribio  nchini  Uingereza.


Barani Ulaya wasi  wasi  unaongezeka  juu  ya  kurejea kwa  virusi, ambapo Ufaransa  inabana vizuwizi, kesi  za  maambukizi  nchini Uingereza zikiongezeka  na  shule  zinafunguliwa  tena katika  kanda ya Ulaya.


China, wakati  huo  huo, imeonesha  chanjo  yake  iliyotengenezwa nchini  humo kwa  mara  ya  kwanza  katika  maonesho ya  biashara mjini  Beijing wiki  hii, na  maafisa  wanamatumaini  kuwa  chanjo hiyo  itaidhinishwa kwa  ajili  ya  matumizi ifikapo  mwishoni mwa mwaka  huu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad